Mp,Ronald karauri akiambatana na Wazili Waelim Ogamba namarafiki wengine Leo talehe 23/1/2026 wamehuthulia hafra .Mang’u High School kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1925

Story by Ayubu John photo journalist from Afrimedia Group.kupitia sherehe kubwa na za kihistoria zilizowaleta pamoja wanafunzi wa sasa, wahitimu, viongozi wa wanafunzi walio kitaifa na wadau wa elimu kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Maadhimisho hayo yaliashiria karne moja ya ubora wa kielimu, uongozi na mchango mkubwa wa shule hiyo katika maendeleo ya taifa.
Tukio lililovutia hisia na gumzo zaidi ni kupokelewa kwa ndege ya Boeing 737-700 iliyotolewa na Kenya Airways kama zawadi ya kipekee ya centenary. Ndege hiyo iliingizwa ndani ya shule baada ya sehemu ya lango kuondolewa ili kuruhusu upitishaji wake. Itatumika kama kituo cha kujifunzia kwa wanafunzi wanaovutiwa na aviation, uhandisi wa anga na teknolojia, hatua inayoimarisha msimamo wa Mang’u kama shule ya ubunifu na maono ya mbele.
Mang’u High School ilianzishwa na Fr. Michael Joseph Witte kama shule ya misheni na baadaye ikakua kuwa mojawapo ya shule bora nchini Kenya, ikijulikana kwa matokeo bora ya KCSE na nidhamu ya juu. Shule hiyo imezalisha viongozi wengi mashuhuri, akiwemo Rais wa zamani Mwai Kibaki, pamoja na viongozi wa sekta za umma na binafsi. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge wa Kasarani, mhitimu wa Mang’u, akiwa ameandamana na CS Julius Ogamba.

Comments

Popular posts from this blog

Little App Launches Air Charter Service, Expanding Access to Private Aviation industry in Kenya

Consortium of August 7 Victims Expresses Frustration After High Court Dismisses Compensation Claims

Savannah Honey Unveils Africa’s First Bee Venom Marketplace