Hotuba ya Kuhusu Soko, Barabara na Mataa

Story by Ayubu John photo journalist Afrimedia Group news 
Mheshimiwa wa Clay City Ward MCA Mwaura Samora amesema. Soko si akaunti ya mtu binafsi. Hata kama baadhi ya watu walinifikisha kortini kuhusiana na soko hili, na sasa tuko mwaka wa pili kortini, niko tayari hata kukaa huko miaka kumi mradi tu wananchi wapate haki yao. Niko tayari kupigania wananchi wa Kirusifi mpaka mwisho.
Nilipigania soko hili lifike hapa kwa manufaa ya watu wa Kirusifi wakati viongozi wengine walishindwa kwa sababu walishirikiana na matapeli. Nilitumia nguvu zote kuhakikisha soko limefika mahali lilipo sasa. Nashukuru Mungu tumepata mkandarasi mzuri na ujenzi uko karibu kukamilika.
Sasa tunapoelekea kwenye ugawaji wa soko, nataka iwe wazi kuwa ugavi hautafanyika kwa upendeleo au kwa simu. Serikali ilibadilisha mfumo wa ugawaji wa masoko. Kutakuwa na kamati rasmi itakayojumuisha watu kutoka Kaunti, Wizara ya Nyumba, na wawakilishi wa mtaa ili kuhakikisha ugavi unafanyika kwa haki na uwazi.
Lengo ni kuhakikisha vibanda vinapewa watu wa eneo hili na wale wanaofanya biashara halali, si watu wa kununua na kuuza vibanda. Tunataka soko lianze kazi mara moja na liwanufaishe wananchi moja kwa moja.
Soko hili litakuwa na nafasi takribani 1,300 za biashara na litasaidia zaidi ya watu 5,000 wa eneo hili. Kutakuwa na hoteli, vijana wa kubeba mizigo, na shughuli nyingi za kiuchumi. Bajeti yake ni takribani shilingi milioni 500, na ni moja ya masoko makubwa zaidi yanayojengwa Nairobi kwa sasa.
Tunamshukuru Rais na Gavana kwa ushirikiano wao. Inatarajiwa kuwa mwezi wa nne au wa tano, Rais atakuja kulifungua rasmi.
Kuhusu Barabara
Tumekuwa na changamoto kubwa ya barabara kwa sababu wakandarasi hawajalipwa kwa wakati. Mfano ni Sutton Road ambayo mkandarasi hakulipwa kwa miaka mitatu na hivyo akasimamisha kazi.
Hata hivyo, tunamshukuru Rais kwa kuidhinisha kilomita moja ya barabara ya lami kwa kila ward Nairobi. Nimeamua kilomita hiyo iwe Sutton Road. Kazi itaanza mara tu zabuni zitakapokamilika, na tunatarajia ndani ya miezi miwili au mitatu barabara iwe imekamilika.
Sutton Road ni mita 500, na mita 500 zilizobaki zitawekwa lami katika barabara ya Mintu wa Badea Rula. Ninafanya kazi kwa manufaa ya kila mtu, si kwa misingi ya eneo la makazi ya mtu yeyote.
Kuhusu Mataa ya Barabarani
Kaunti imekuwa na changamoto ya kununua vifaa vya kutengeneza na kuweka mataa. Rais pia ameahidi kuwa kila ward itapata mataa 100.
Mataa hayo yatawekwa katika maeneo yenye changamoto kama Keroka, Maji Mazuri, Hunters, na Visos ili kuboresha usalama.
Kwa ujumla, lengo letu ni kuhakikisha maendeleo yanafanyika kwa haki, uwazi na manufaa ya wananchi wote.
Asanteni sana. Mungu awabariki

Comments

Popular posts from this blog

Little App Launches Air Charter Service, Expanding Access to Private Aviation industry in Kenya

Consortium of August 7 Victims Expresses Frustration After High Court Dismisses Compensation Claims

Savannah Honey Unveils Africa’s First Bee Venom Marketplace